Watendaji wa kata, Waganga Wafawidhi, na Wakuu wa shule mbalimbali Msingi na Sekondari pamoja na wasaidizi wao wamekutanishwa pamoja katika Chuo cha Ualimu Tukuyu lengo likiwa ni kujengewa uwezo dhidi ya Mfumo wa Manunuzi (NesT) ambao pamoja na mambo mengine mfumo huu unatoa fursa ya manunuzi yote ya Serikali kufanyika kwa njia ya Kielektroniki.
Mafunzo yamefunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Rungwe bwana Adamu Salum
Mfumo huu ambao umeendelea kutekelezwa nchi nzima umeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Manunuzi huku ukiondoa vitendo vya rushwa, utunzaji wa kumbukumbu, usawa na uwazi katika kupata kazi kwa wazabuni, uharaka wa manunuzi na mengine mengi.
Mkuu kitengo cha Manunuzi Bi Milly John Massare ameeleza kuwa Kuhitimishwa kwa mafunzo haya kutasaidia Manunuzi yote kufanyika kwa wakati hasa katika miradi ya maendeleo, kuondoa urasimu katika mnyororo wa manunuzi pia kuwaoondolea adha watalamu katika maeneo yao ya kazi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya usaidizi katika mfumo wa manunuzi.
Mafunzo haya yatadumu kwa muda wa siku mbili huku yakiwahusisha pia watalamu kutoka PPRA
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa