Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. David Silinde amefanya ziara katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe leo asubuhi tarehe 20.12.2021 Kwa kukagua miradi ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya COVID 19.
Katika ziara hiyo ametembelea shule ya Sekondari Kinyala na Ndembela one zikiwa ni kati ya shule 18 zinazonufaika na mpango huu ambapo jumla ya vyumba 55 vinajengwa kwa thamani ya shilingi Billion 1.1
Akiwa katika shule ya sekondari Kinyala Mhe. Silinde amesifu mradi unavyoendelea kutekelezwa kwa viwango vinavyokubalika huku akiagiza kumilisha ujenzi huo kabla ya Disemba 31 mwaka huu.
Aidha amewapongeza wakazi wa kata ya Makandana kwa kuanzisha shule mpya ya Sekondari Ndembela one na kuijenga kwa viwango stahiki huku akiahidi serikali kuendelea kuleta fedha nyingine kwa ajili ya vyumba vya madarasa na miundombinu mingine.
Wakati huohuo ameagiza uongozi wa kata na shule hiyo kuendelea kutunza majengo ya shule hiyo ili yaendelee kunufaisha vizazi vijavyo ambapo ameongeza kuwa sehemu nyingi hapa nchini baada ya miradi kukamilika majengo yamekuwa yakiachwa bila kukarabatiwa na hivyo kukosa ubora wake.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt. Vicent Anney ameahidi mbele ya Naibu Waziri kuwa miradi yote itakamilika kwa wakati huku akiiomba Serikali kuipa kipaumbele Shule Mpya ya Sekondari Kyobo kwa Kuipatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za walimu kutokana na changamoto ya umbali na hivyo kuwa na mazingira rafiki ya kuishi na kufundisha.
Naibu Waziri ataendelea na ziara katika Halmashauri ya Busokelo na Kyela.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa