BITEKO AFANYA ZIARA RUNGWE
Naibu Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dotto Biteko amefanya ziara leo tarehe 20.2.2024 na kukagua miradi ya uendelezaji wa umeme wa joto ardhi katika eneo la Kyejo Mbaka pamoja Ngosi ikiwa ni hatua ya kuongeza upatikanaji wa umeme nchini Tanzania.
Mhe. Biteko ameridhishwa na kiwango cha ujenzi kilichofikiwa na kuwa miradi hii itakapokamilika itaongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme nchini na hivyo kuongeza kiwango cha Uchumi kwa wananchi
Mradi wa Kyejo unatarajia kuzalisha kiwango cha Megawati 60 huku Ngosi iliyopo kata ya Isongole ikitoa Megawati 70
Mhe. Biteko amewatoa hofu watanzania dhidi ya kukatika katika kwa umeme na kuwa hali hii inatokana na ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme ambapo kwa sasa hatua nzuri imefikiwa huku Mashine zimeanza kufungwa katika Bwawa la Nyerere ambalo litaondoa adha yote ya uhaba wa umeme nchini.
Aidha ameeleza kuwa Serikali imekuwa ikitekeleza miradi mingine ya umeme kama ,gesi, pamoja upepo ambayo yote itaongeza umeme hasa vijijini ambako umeme umepelekwa kuchachusha uchumi wa wananchi kupitia Mpango wa REA.
Katika hatua nyingine amewahimiza Wakazi wa Wilaya ya Rungwe kujitokeza kwa wingi katika zoezi la Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu, huku wakidumisha amani na utulivu silaha waliyotuachia waasisi wa taifa hili.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa