Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Julius Chalya (kulia) akitoa maelezo ya chanzo cha maji (Intake) Masomo group kichopo katika mto Mbaka mbele ya Naibu Waziri wizara ya MAJI Mhe. Maryprisca Mahundi ambapo imeelezwa kuwa mradi huo mpaka sasa umevinufaisha vijiji 18 katika kata ya Masoko, Masukulu na Itagata.
Aidha Mhe. Mahundi amewaomba wananchi wanaozunguka chanzo hicho kuendelea kukitunza ili kiendelee kukinufaisha kizazi hiki na kijacho.
" Mradi huu ni mkubwa sana ni vema uendelee kupanuliwa ili vijiji vingi vinufaike zaidi na hii itawezekana ikiwa tutaendelea kukitunza chanzo hiki" Amesisitiza.
Hata hivyo amemuomba mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi Mbeya ( MBEWASA) kumpa mapendekezo namna ya kuboresha upatikanaji wa maji katika mji Tukuyu ndani ya wiki moja ili kuongeza kasi ya utoaji wa huduma hiyo Kwa wananchi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa