Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Tamisemi Ndugu Wilson Charles Mahela pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Grace Maghembe Wamefanya ziara leo tarehe 14.7.2023 na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) ghorofa moja katika Hospitali ya wilaya Tukuyu.
Ndugu Mahela amepongeza kwa hatua iliyofikiwa na kuwa kumalizika kwake kutaongeza ufanisi wa matibabu katika hospitali hii.
Ndugu Mahela katika maeneo tofauti amepongeza kwa Halmashauri kufanikiwa kupunguza tatizo la Udumavu kwa watoto mpaka kufikia asilimia 18% huku vitendo vya ukatili kwa watoto vikizidi kupungua katika jamii na hivyo kupanua ustawi wa jamii.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa