-NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII- NJOO UIONE
Ipo dhana potofu katika jamii kuwa zipo kazi ambazo Wanawake hawaruhusiwi kuzifanya na kuwa zimetengwa kwa ajili ya wanaume tu.
Stela Seme (28) Mama na mkazi wa Kijiji Cha Ntokela tarafa ya Ukukwe ameweka kando Imani hiyo.
Stela ambaye ni mke na mama mwenye watoto wawili anaeleza kuwa shughuli ya ujenzi aliianza kama fundi msaidizi mwaka 2018 jijini Mbeya nafasi iliyo mpa fursa ya kupata ujuzi na maarifa ya namna ya kujenga nyumba kutoka hatua msingi mpaka ukamilishaji.
Anaeleza kuwa awali aliona kazi ngumu huku akikatishwa tamaa na rafiki zake lakini kwa kuwa alikuwa na malengo mahususi na kazi yake ndoto yake ilitimia.
Stela Seme Sasa ni fundi makini na mwenye weledi wa kufurahisha.
"Niliambiwa kazi hiyo ngumu, unaacha kazi ya kuuza viazi unakimbilia kujenga! hakika hutaweza. Lakini sikuwasikiliza. Ameeleza Stela.
Ujuzi alioupata umemuwezesha kushiriki ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbeya, na Kituo Cha afya Ndanto ambapo anaendelea na hatua ya ujenzi jengo la kufulia.
Aidha ameshiriki kujenga nyumba mbalimbali jijini Mbeya , Songwe na Rungwe.
Stela anaeleza kuwa kazi hiyo imemnufaisha kwa kumuwezesha kujenga nyumba yake ya Kuishi, kununua mashamba na kusomesha watoto.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa