Mwongozo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) Ulioboreshwa wa mwaka 2019 umezaa matunda baada ya wakazi wa kijiji cha Mpuga kata ya Kisondela kukarabati shule ya Msingi Lutengano ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu kwa wanafunzi.
Kupitia mwongozo huu wananchi wanajengewa uwezo wa kubuni na kushiriki katika fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Kupitia O&OD Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imekuwa ikihamasisha wananchi kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata mbalimbali ambapo katika kijiji cha Nzunda kata ya Ndanto wakazi wake wamejenga soko, ofisi ya kijiji, mradi wa maji, pamoja na zahanati.
Aidha vijiji vingi pia vimehamasika katika ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, maji, barabara na kilimo.
Mathalani wakazi wa kata ya Swaya wameanza ujenzi wa kituo cha afya huku serikali ikiwaunga mkono katika hatua mbalimbali.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa