Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga ameagiza wazazi/ walezi kuendelea kuchangia chakula shuleni kikiwa katika hali ya ubichi/ kisichopikwa ikiwa ni jitihada ya kupunguza matatizo ya magonjwa ya matumbo/ kuhara kwa wanafunzi tatizo linalosababishwa na wazazi kuwafungashia watoto chakula kilichochacha " kiporo".
Aidha amesisitiza wazazi kuhakikisha wanachangia vyakula vyenye viini lishe tofauti ili kuongeza afya ya mwili sambamba na kupandisha kiwango cha ufaulu katika masomo yao.
Baadhi ya vyakula vinanyopatikana wilayani Rungwe ni pamoja na Mahindi, Maharage, Viazi, magimbi, Maziwa, Njegere, Machungwa, mawese, karanga, mananasi, ndizi, mihogo, karoti, mboga za majani, nyanya chungu, nyanya, bamia, maparachichi, mapera na vingine vingi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa