Chama cha Wanawake Mawakili Tanzania ( TAWLA) leo mapema tarehe 02. 6. 2021 mbele ya Wakuu wa Idara kimeutambulisha mradi wa Mwanamke Imara katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe utakaolenga kumjengea jukwaa imara la kumlinda msichana na Mwanamke dhidi ya ukatili wa kijinsia, kutoa fursa za uongozi katika jamii, kutoa haki Kwa wakati, na kutoa fursa za kiuchumi Kwa wasichana na Wanawake Kwa Maendeleo endelevu.
Katika hatua za awali mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika kijiji cha Bugoba kata ya Kisondera Kwa kuwashirikisha wakazi wa maeneo hayo kwa kuunda Sheria ndogondogo zitakazo saidia kumjengea mazingira rafiki na nadhifu ya majukumu yake ya kila siku.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa