Mtandao wa Wanawake wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (National Networking Women Living With HIV in Tanzania) umewakutanisha vijana mashujaa wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo kutoka katika vijiji sita katika kata ya Kisondela, Kyimo, Isongole, Makandana, na Ndanto.
Dhima kubwa ya mtandao huu ni kuhakikisha unawafikia vijana balehe ukilenga kutoa elimu ya afya ya uzazi na kinga dhidi ya maambukizi ya HIV.
Akitoa takwimu za maambuki ya UKIMWI Katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe; Mratibu wa Halmasahauri Bwana George Mashimba ameeleza kuwa jumla ya wakazi 12,158 wanaishi na Virusi vya UKIMWI.
Kati ya hao wakazi 659 ni vijana huku Wanawake wakiwa 467 na Wavulana 192.
Hatua hii ya kuongezeka kundi kubwa la vijana wanawake limeusukuma mtandao huu kuona namna bora na sahihi ya kulinasua kundi hili muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Mradi utawafikia vijana balehe wanawake wanaoishi katika mazingira hatarishi mathalani wale wanaojiuza katika maeneo mbalimbali na kumbi za starehe .
Mkurugenzi wa Mradi huu Bi. Veronika Lyimo ametaja mikakati ya kuwafikia vijana hawa kuwa ni pamoja kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na mashujaa wawili wanaoishi na Virusi vya Ukimwi huku wakitoa elimu namna ya kujikinga na Maambukizi, matumizi ya dawa za kufubaza virusi, pamoja Ulaji wa chakula lishe kila wakati.
Vijana hawa 12 katika vijiji sita watasaidia kuwafikia wanawake wengine zaidi ya 300 katika wilaya ya Rungwe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa