Mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi katika kata ya Ndanto yameendelea kwa wiki moja mfululizo.
Mafunzo hayo yanayotolewa na mradi wa PS3+ Chini ya wizara ya TAMISEMI kwa ufadhili wa watu wa Marekani yamelenga kuwajengea uwezo Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji, Walimu wakuu na Mkuu wa shule na kamati zake,wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya na kamati zake .
Kata ya ndanto ina jumla ya vijiji vinne, shule za msingi tano, sekondari ya umma moja na zahanati mbili.
Mafunzo hayo pia yameendelea pia kwa watendaji wote katika kata zote 29
Katika mafunzo hayo viongozi wamejengewa uwezo dhidi ya utawala bora ikilenga namna ya uendeshaji wa vikao, uandishi wa mihutasari ya vikao, Ushiriki wa wananchi katika kuandaa bajeti, Kusomewa mapato na Matumizi, Matumizi ya mbao za matangazo, radio za kijamii, Tovuti ya Halmashauri yakiwa kama majukwa mahususi ya kutolea taarifa za maendeleo katika maeneo yao.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufungwa siku ya jumamosi tarehe 13.05.2022 na baada ya hapo yataendelea katika vijiji vyote katika kata 29 kwa watendaji wa kata kutoa mafunzo wakishirikiana na Watendaji kutoka ngazi ya Halmashauri
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa