Picha hapo ni Mwananchi wa Kitongoji cha Syukula Bwana Almasi Kibuta akihojiwa na Philip Mwihava, Mtangazi wa kituo cha Redio cha Cloud Fm cha jijini Dar es salam.
Bwana Mwihava amejifunza mengi dhidi ya Utawala bora, Ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo na namna walivyohamasika kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa- ICHF.
Mradi wa PS3+ chini ya ufadhili wa watu wa Marekani mapema mwezi wa kwanza mwaka huu umetoa kiasi cha fedha kwa ajili ya ufadhili wa vipindi vya redio kupitia redio Rungwe iliyopo mjini Tukuyu.
Kupitia redio hii wakazi wa Wilaya ya Rungwe na maeneo ya jirani waliweza kusikiliza vipindi vya namna ya kujiunga mfuko wa bima ya afya, Mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Utawala bora, Wananchi kujihusisha na shughuli za maendeleo na vingine vingi.
Bwana Almasi Kibuta alisikiliza Redio Rungwe FM 102.5 Mhz na kuhamasika kujiunga na Mfuko wa Bima ya afya iliyoboreshwa. Awali kabla ya kujiunga na mfuko huu alikuwa anatumia gharama nyingi kupata matibabu lakini baada ya kupata elimu alilazimika kutafuta shilingi 30,000/= zilizomsaidia kupata kadi ya bima pamoja na wanufaika wengine watano.
" Bima ya afya ni mlinzi wa akili yangu kwani mara ninapougua sihangaiki sana namna ya kupata matibabu zaidi ya kuwaona watalamu wa afya na kutibiwa haraka" ameongeza bwana Kibuta.
Naye Bi mkazi wa mtaa wa Magereza kata ya Kawetere amezidi kuwahamasisha wakazi wengi wilayani Rungwe kujiunga na mfuko huu kwani yeye ilimchukua siku moja tu kupata kitambulisho cha Bima ya afya na tayari amepata faida Lukuki.
Kwanza akiwa kama mama mlezi wa familia bima hii inamsaidi kuwaweka watoto wake katika hali ya usalama na ustawi mzuri wa afya zao lakini pili imemuimarishia uchumi kwani baadala ya fedha zake kutumika kwenye matibabu Bima imekuwa ngao yake na fedha zake amezielekeza katika vitega uchumi vingine.
Aidha Kijiji cha Nzunda kata ya Ndanto kimenufaika na elimu ya utawala bora.Kwa kutumia miongozo ya utawala bora kijiji kimeweza kuitisha mikutano ya mara kwa mara, kusoma mapato na matumizi, Kuweka matangazo katika ubao wa matangazo na kuwahamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Mtedaji wa kijiji hicho ameeleza kuwa kwa kwa kutumia mapato ya ndani, kijiji kimeweza kujenga ofisi ya kijiji iliyogharimu shilingi Million 38 ujenzi wa soko la kisasa unaoendelea unaotarajia kugharimu kiasi cha shilingi million 100 ujenzi wa mradi wa maji uliogharimu shillingi million 103 na uchimbaji wa barabara katika mitaa yao.
Hii ni faida ya ushirikiswaji wa wananchi.Kwa kutumia uongozi wa kata na Halmashauri kwa ujumla vijiji vingi vimehamasishwa kuhakikisha shughuli za utawala bora zinatekelezwa ikiwa ni nyenzo pekee ya kuleta maendeleo katika maeneo yao sambamba na kuleta amani na utulivu.
Mradi wa PS3+ toka uanze kufanya kazi katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe umeisaidia kuijengea jamii dhidi ya mambo mengi yanayowazunguka hali hii imeendelea kuwahasisha kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa