Chuo kikuu cha kilimo sokoine kilichopo mkoani Morogoro kimekabidhi leo tarehe 12.11.2021 mradi wa malisho ya ng'ombe (Bracharia) kikilenga kuongeza kiwango cha uzalishaji wa maziwa sambamba na kuinua kipato kwa wakulima.Makabidhiano hayo yamefanyika katika kituo cha kilimo na mifugo kijiji cha Ilenge kata ya kyimo.
Akipokea mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Afisa kilimo na uvuvi Bwana Augustino Lawi ameomba wafugaji katika wilaya ya Rungwe kuendelea kutumia malisho yaliyoboreshwa ili kujenga lishe bora kwa wanyama na kueneza elimu waliyoipata kwa wafugaji wengi zaidi ili kuongeza kiwango cha maziwa na nyama na hivyo Rungwe kuwa kitovu cha mifugo bora mkoani Mbeya na taifa kwa Ujumla.
Hata hivyo Mratibu wa mradi wa InnovAfrika Profesa Dismas Mwaseba ameshukuru wafugaji kwa ushirikiano waliouonesha na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano mara utakapohitajika
Katika makabidhiano hayo wafugaji kadhaa walishuhudia ambapo Bwana Hosiana Mwakanjwanga mfugaji kutoka Nsongwa amearifu kuwa baada ya kuanza kutumia majani hayo uzalishaji wa maziwa umeongezeka kwa wastani wa lita 20-25 kwa ng'ombe mmoja tofauti na awali ambapo alikamua lita 10 tu kwa siku.
Mbegu za malisho haya zinapatikana katika ofisi za kilimo na mifugo Halmashauri ya wilaya ya Rungwe huku vipando vikipatikana pia katika shamba darasa lililopo katika kituo cha kilimo na mifugo Ilenge, Shamba la malisho ya mifugo kalalo kata ya Lufingo na kupitia mashamba ya wafugaji mbalimbali walioenea kona zote wilaya ya Rungwe
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa