KIMSINGI KUISHI RUNGWE NI FURAHA TELE.
Mlima Rungwe ni fahari kwa wakazi wa mikoa ya nyanda za juu kusini.
Mlima Rungwe hubeba jina la Wilaya ya Rungwe ambayo makao makuu yake yapo Tukuyu na ndiyo wilaya kongwe zaidi katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Mlima Rungwe huchangia asilimia 49% ya maji yote katika ziwa Nyasa.
Mito mikubwa ambayo chanzo chake ni Mlima Rungwe ni pamoja na Kiwira, Lufiliyo na Mbaka. Mito yote hii hutiririsha maji Kuelekea ziwa Nyasa.
Huu ndiyo mlima mrefu zaidi kwa mikoa ya nyanda za juu kusini.
Mlima Rungwe una urefu wa mita 2981 kutoka usawa wa bahari.
Maji yanayotiririka Kuelekea ziwa Nyasa ndiyo huchangia uzalishaji wa chakula hasa kilimo cha Mpunga katika wilaya ya Kyela.
Katika hatua hiyo utalii wa ziwa Nyasa huchangiwa sehemu kubwa na uwepo wa mlima Mlima Rungwe.
Ndiyo maana wakati wa majira ya joto kali enzi za Ukoloni, Watawala , Wamishionari pamoja na familia zao (Wanaoishi Mwambao mwa ziwa Nyasa ; Kyela na Ludewa) walitumia muda wa Mapumziko kupanda Mlima Rungwe na Kupiga kambi katika eneo la Isongole fishing camp lililopo katika Mzizi (Chini) ya Mlima Rungwe.
Haya ni maeneo yenye baridi ya wastani, mvuto wa kipekee na msitu mnene.
Wastani wa watalii 2000 hupanda mlima Rungwe kila Mwaka.
Baadhi ya nchi kama Malawi na Zambia zimewahi kufanya ziara na kujifunza namna ambavyo Serikali kwa kushirikiana na Wananchi wameweza kutunza na kuhifadhi msitu wa Mlima Rungwe.
Mlima Rungwe husimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania Mount Rungwe Nature Reserve na ofisi zake zipo Ndyonga Tukuyu Mjini barabara ya Tukuyu -Busokelo.
Zipo fursa mbalimbali za Uwekezaji kando ya Mlima Rungwe. Hizi ni pamoja na kambi za watalii, Hoteli, Kilimo, Viwanda vya maji, na uchakataji wa bidhaa za shambani.
Tayari Hoteli na kambi zimeanza kujengwa(Newland, Kalongo farm, Mbutusyo, Landmark n.k), Mashamba makubwa ya chai na parachichi, Viwanda vya maji (Tukuyu spring water na Rungwe water ) nakadhalika.
Hujachelewa Karibu Rungwe!!!!!
Karibu Rungwe wekeza nasi kupitia www.rungwedc.go.tz
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa