Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Albert Chalamila afanya Ziara katika Wilaya ya Rungwe Leo tarehe 13/09/2018. Ziara hiyo ikiwa ni ya kwanza katika Wilaya ya Rungwe tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Joseph Magufuri mnamo tarehe 29/07/2018.
Ziara hiyo alianza kwa kuongea na Watumishi wa Umma waliopo Makao Makuu ya Wilaya ya Rungwe,mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Tukuyu mjini. Baada ya kumaliza mkutano huo na Mkuu wa Mkoa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Wilaya walienda kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa Chuo cha Ualimu Mpuguso, mradi huo umegharimu kiasi cha tsh.bilioni 9.6.
Aidha baada ya kumaliza ukaguzi huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alifanya mkutano wa hadhara na Wananchi katika Uwanja wa Tandale uliopo Tukuyu mjini ambapo katika mkutano alijtambulisha na kuwasisitiza kila mmoja anapaswa kuwajibika vema katika nafasi yake. Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya aliwasihi wananchi kufikisha malalamiko,kero,maswali na mahitaji katika ofisi za umma ikiwa ni pamoja na Ofisi yake.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa katika mkutano huo aliwataka na kuwaomba Wananchi wawe wanajitokeza katika mkutano hiyo ili kutoa taarifa,malalamiko,maoni ,maswali ili kupata majibu sahihi kutoka kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alisisitiza Wananchi kuwa na ushirikiano na viongozi katika kujenga na kuleta maendeleo katika Wilaya ya Rungwe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa