KARIBU RUNGWE MHE.JAFFAR HANIU
Mkuu Mpya wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar amekabidhiwa rasmi jukumu la kuongoza Halmashauri mbili ambazo ni Rungwe na Busokelo.
Hizi ndizo zinaunda Wilaya ya Rungwe huku Bosokelo ikiwa na kata 11 tarafa Moja na Rungwe ikiwa na kata 29 na tarafa tatu.
Akikabidhi Ofisi, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Dkt Vicent Anney ambaye Sasa amehamia Wilaya ya Bunda Mkoani mara ameeleza mafanikio kadhaa yaliyopatikana.
1.Kumeanzishwa viwanda vidogo na vidogo vya kuchakata bidhaa za kilimo na Mifugo.
2. Ufaulu umeongezeka kwa shule za Msingi na Sekondari huku Rungwe ilifaulisha mpaka kufikia asilimia 93.7%.
3. Uandikishaji wa wanafunzi kwa darasa la awali na darasa la kwanza umepanda mpaka kufikia asilimia 100% mpaka kufikia January 30 mwaka huu.
3.Upatikanaji wa maji safi na salama umeongezeka akiutaja Mradi wa Masoko group unaoenda kuzinufaisha kata zaidi ya tisa ikiwemo Tukuyu mjini.
4.Vyumba vya madarasa vimeongezeka ambapo kwa Busokelo na Rungwe ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2022 jumla ya vyumba 20 vilijengwa.
5. Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilipanda mpaka kufikia nafasi ya 8 kati ya Halmashauri bora nchini
6. Miundombinu ya Barabara, na umeme imeendelea kuimarishwa .
Naye Mkuu Mpya wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu ameomba ushirikiano ili kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa na mtangulizi wake sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama tawala na taifa Kwa ujumla.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa