Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau amefanya kikao kifupi na watumishi wa Halmashauri ya Rungwe huku akiwaomba kuendelea kushirikiana ikiwa ni pamoja na kushikamana ili kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na hivyo kuwaletea maendeleo endelevu.
Aidha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji ambaye kwa sasa amehamishiwa katika Halmashauri ya Busokelo Bi. Loema Peter amewashukuru watumishi pamoja na wakazi wote wa wilaya ya Rungwe katika kipindi chote alichokuwepo kwa ushirikiano aliopewa ambapo miradi kadhaa imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa sambasamba na Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na watalamu hali iliyochochea amani na utulivu kazini.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa