MINYOO TEGU YATEGULIWA RUNGWE
Mradi wa Cystinet Afrika kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA) umewasilisha leo matokeo ya utafiti wa Minyoo Tegu katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Utafiti umefanyika katika vijiji vinavyopatikana katika kata ya Mpuguso na Kisiba.
Wilaya zingine zilizotafitiwa ni pamoja na Mbinga, Kongwa, Mpwapwa, Babati na Nyasa.
Minyoo tegu inayopatikana katika mwili wa Binadamu na Nguruwe huambukizwa kwa mnyoo kutoka kwa binadamu kwenda kwa nguruwe kutokana na kula kinyesi cha binadamu au mabaki ya chakula kuliwa na nguruwe au binadamu kula nguruwe aliyeathiriwa na minyoo hii.
Utafiti umebaini kuwa ukosefu wa elimu na kushindwa kubadili tabia hatarishi imekuwa kichocheo cha maambuki ya minyoo hii.
Minyoo hiyo imekuwa ukiathiri sehemu ya ngozi ya binadamu na sehemu ya ubongo wa binadamu na kusababisha kifafa.
Utafiti uliofanywa nchini Tanzania umebaini kuwa mnamo mwaka 2012 Tanzania ilitumia takriban dola za kimarekani Million 5 kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa kifafa kinachotokana na minyoo ya Tegu na dola 3 kwa ajili ya gharama ya kuteketeza nyama ya nguruwe yenye vimelea vya minyoo hiyo.
Sababu zifuatazo ni kichocheo cha minyoo tegu:
1.Kunywa maji yasiyo salama
2.Kaya kutokuwa na choo au choo kisicho salama.
3.Kujisaidia maeneo yaliyobaki
4.Kutonawa maji kabla ya kula chakula baada ya kutoka chooni.
5.Kutoosha mboga na Matunda kabla ya kula.
6.Kutopika nyama ya nguruwe ipasavyo
7.Uchinjaji wa nyama ya nguruwe bila kibali cha mtaalamu.
8.Kuuza nyama ya nguruwe yenye minyoo ya Tegu.
Mamlaka na jamii zimeendelea kukumbushwa kuhakikisha taratibu na kanuni za usafi zinafuatwa sambamba uzingatiaji wa ulaji na usambazaji wa nyama ya nguruwe kwa kufuata maelekezo ya watalamu wa afya na mifugo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa