Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe inatakeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika uwezeshaji wa wanawake, vijana na walemavu kiuchumi kwa kuwapatia mikopo isiyokuwa na riba kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019. Masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ni moja ya maeneo ya msisitizo katika malengo ya maendelo endelevu ya hadi mwaka 2030 katika ushiriki wa wananchi katika shughuli za uchumi. Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe itaendelea kuweka mikakati ya kuwezesha wanawake, vijana na walemavu kiuchumi.
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imetoa mkopo kwa Robo ya pili Octoba –Desemba 2018/2019 tarehe 5/2/2019 katika Ukumbi wa Halmashauri mkopo huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi Loema I.Peter baada ya kukagua kazi zinazofanywa na wanavikundi katika uendeleza wa viwanda vidogovidogo kisha ukabidhi mikopo kwa vikundi 13 vinavyojishughulisha na viwanda vidogo vidogo jumla ya Tshs 74,900,000/= Idadi ya wanufaika wa mkopo huu ni 294, pamoja na shughuli hiyo ya utoaji mikopo pia aliwakabidhi wajasiliamali wadogo vitambulisho vya biashara vilivyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, fedha hizo ni kutokana na makusanyo ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya Tshs 40,000,000/= na marejesho ya mfuko wa wanawake na vijana kwa amana ya mikopo na riba 34,900,000/.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji aliwasisitiza fedha hizo zilizotolewa zitafautiliwa hivyo wakazitumie katika matokeo chanya ili kuleta maendeleo ya uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Mkurugwnzi huyo aliwaeleza wanavikundi hao fedha hizo zinatakiwa zirudi kama zilivyo kwa kuzingatia muda waliokubaliana na kusaini katika mikataba yao,pia urudishaji wa fedha hizo unasaidaia kukopesha tena kwa vikundi vingine au kuongezewa kiasi kikubwa cha mkopo.
Aidha alisisitiza zaidi kwa wanufaika hao kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa kusema "sitaona shida kwa vikundi vyenye shughuli za kiviwanda na ambao wanafanya vizuri kuwaongezea kiwango cha mkopo mkubwa" aidha aliwaeleza kuwa mikopo hiyo haina riba na serikali imepitisha sheria hiyo kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019."
Baada ya kukabidhi mikopo hiyo na vitambulisho wanufaika walishukuru serikali kwa kuwainua kiuchumi kwa kuwapa mikopo hiyo maana imesababisha na kina mama kuinuka kiuchumi na hivyo katika familia nao wamekuwa na mchango mkubwa na kuthaminika zaidi hivyo familia nyingi zimekuwa na amani na furaha,pia waliishukuru serikali kuwaondolea riba katika mikopo hiyo na kuahidi kuizalisha zaidi na kurejesha kwa wakati mikopo hiyo.
Shughuli ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana ni endelevu kwa kila robo. Aidha Robo ya kwanza Julai-Septemba 2018/2019 jumla ya Tshs 74,500,000/= zilitolewa, ambapo 50,500,000/= zilitolewa kwenye vikundi 7 vya wanawake na Tshs 24,000,000/= zilitolewa kwenye vikundi 6 vya vijana.
(pichani Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi.Loema I.Peter akitoa hati kwaajili ya Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake,Walemavu na Vijana na kukabidhi vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo.)
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa