ASILIMIA 10% YAWANUFAISHA VIJANA KIWIRA
Halmashauri (W) Rungwe imetoa kiasi cha shilingi Million 30 kwa kikundi cha vijana Ndabhalo kilichopo Mpandapanda kata ya Kiwira ikiwa ni asilimia 10% ya Mapato ya ndani fedha ambayo hutengwa kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango imekagua mradi huu na kuridhishwa na ufugaji unaondelea
Kikundi hiki cha Ndabhalo hujishughulisha na ufugaji wa ngombe ambapo mpaka sasa wamenunua ng'ombe nane mpango ukiwa ni kufikisha mpaka ng'ombe 10.
Fedha hizi hutolewa kila robo ya mwaka na hurejeshwa bila riba.
Mikopo kama hii imesaidia kuwajengea wananchi uwezo kiuchumi na hivyo kupanua kipato chao na hivyo kujinasua katika makucha ya umasikini.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa