Katika robo tatu mwaka 2021/22, kikundi cha Edeni kilichopo katika kata ya Ilima kilikopeshwa Jumla ya shilingi million 8 na Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ukiwa ni mkopo usio na riba unatokana na asilimia 10% ya mapato yake ya ndani.
Kikundi hicho chenye jumla ya vijana 16 kilinunua vifaa vya useremala na kubahatika kuliteka soko zima la kata hiyo.
Kutokana na kukua kwa mtaji, kikundi kimeweza kuajiri vijana wengine wanne kutoka Arusha ikiwa ni sehemu ya kuchavusha maarifa na ujuzi wa kikundi.Kwa Sasa kikundi kinatarajia kumaliza marejesho mwishoni kwa mwezi juni mwaka huu
Kikundi hicho kina kinachijishughukusha pia na kilimo cha mbogamboga na matunda kimemeweza kutengeza samani na kuzisambaza katika shule, vyuo, nyumbani na taasisi za kidni.
Mwenyekiti wa kikundi hicho bwana Shadrack Hamza ametaja kuwa kwa sasa wapo mbioni kuanzisha katakana kubwa na hivyo kuwa kiwanda cha mfano katika ukanda huu.
Katika zoezi hili la anuani za makazi na Postikodi linaloendelea kikundi hiki kimejinyakulia zabuni ya kutengebeza vibao kwa nyumba zote katika kata hii na hivyo kupanua wigo wa MAPATO ya kikundi hiki
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa