Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara leo tarehe 07.8.2022 katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Katika ziara hiyo amezindua majengo ya Chuo Cha Ualimu Mpuguso yaliyogharimu kiasi Cha shilingi Billion 10 fedha iliyotolewa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Kanada.
Aidha Mhe.Rais ameagiza uongozi wa chuo hicho kuendelea kuyatunza majengo hayo ili yakinufaishe kizazi kijacho na hivyo kuunganisha mnyororo wa maarifa na ujuzi nchini.
Awali akizungumza na wakazi wa kata yaKiwira Mhe. Rais ameahidi kutoa kiasi Cha shilingi Million 10 kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa kituo cha afya huku akiagiza wizara ya TAMISEMI kuangalia uwezekano wa kupekeka fedha zaidi kwa ajili ya ukamilishaji wa kituo hicho.
Wakati huhuo Waziri wa ujenzi Mhe. Makamu Mbarawa ameeleza kuwa serikali ipo mbioni kuweka taa za Barabarani kwa urefu wa km 2 katika mji wa Tukuyu na Kiwira kwa gharama ya shilingi million 200 hali itakayoimarisha Usalama sambamba na kufanya biashara usiku na mchana.
Katika hatua nyingine waziri wa kilimo Mhe. Hussein Bashe amearifu kuwa katika msimu huu Serikali imetoa ruzuku kwa asilimia 50% katika pembejeo ya mbolea aina zote hali itakayochavusha mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo na hivyo kuinua kipato na uhakika wa chakula kwa kila kaya na nchi kwa ujumla.
Naye waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji amesema kuwa serikali inandaa mfumo mpya wa soko la parachichi ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha bei ya zao hilo huku akiwaomba wakulima kutembelea viwanja vya Nanenane jijini Mbeya ili kupata maelekezo na mkopo wa mashine za kukamlia mafuta ya matunda ya parachichi zinazotolewa kwa gharama nafuu.
Akihitimisha ziara hiyo Wilayani Rungwe Mhe.Rais ameushukuru uongozi wa Wilaya ya Rungwe kwa kuendelea kulinda amani na utulivu, kusimamia miradi kikamilifu na kuwaomba wakazi wa Wilaya hii kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi agosti 23,2022 ili kuipa nafasi Serikali kupanga mipango endelevu na yenye tija kwa watu wake.Ziara imeendelea Wilayani Kyela ambapo atazindua miradi kadhaa pamoja na kuzungumza na wananchi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa