Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilipokea Mwenge wa Uhuru tarehe 07/09/2019 na kukabidhi kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya tarehe 8/09/2019. Mwenge wa Uhuru ulikagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Miradi hiyo ya kisekta za Elimu, Maji, Barabara,Utawala, Afya, Mapambano dhidi ya Ukimwi, Mapambano dhidi ya Rushwa,Kilimo,Viwanda na Uwekezaji, shughuli za uinuaji kiuchumi kwa Wanawake, Watu wenye Ulemavu na vijana.
Aidha shughuli zilizofanyika ni kukagua vyumba vinne vya madarasa na chumba kimoja cha Ofisi shule yaSekondari Kayuki, Kuzindua Ofisi ya kata ya Kawetele,Kuweka jiwe la msingi Barabara ya Bomani -Msasani, Uzinduzi wa Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Elimu, Kuweka Jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha maji, Kukagua Mradi wa maji Lugombo,Kutembelea Kilimo cha kitalu nyumba, Kuzindua Ghala baridi la matunda,Kukagua vikundi vitatu vya wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu vilivyopewa mkopo na Halmashauri 2018, kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Kiongozi wa Mwenge wa Kitaifa Ndugu Mzee Ali Mkongea alitoa pongezi kwa Halmashauri kwa mapokezi na maandalizi mazuri ya miradi yenye tija kwa jamii na kusisitiza miradi hiyo iliyowekwa mawe ya msingi imalizike na iliyozinduliwa itunzwe vizuri.
Jumla ya miradi 11 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ina thamani ya tsh 7,789,098,138.72.
Baadhi ya picha za matukio katika Mbio za Mwenge wa Uhuru
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa