MAWASILIANO KATI YA KAPUGI - LYENJE IKUTI YAKATIKA
Kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha; Barabara ya Kapugi-Lyenje Ikuti kupitia Mto Kiwira imekatika na hivyo kuondoa Mawasiliano kati ya Vijiji hivi Viwili.
Leo tarehe 16.4.2024 Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu amefika katika eneo la tukio na kukagua madhara yaliyojitokeza huku kupitia vyombo vya Habari akiomba wakazi wa Wilaya ya Rungwe kuendelea kuchukua tahadhari dhidi majanga haya katika kipindi hiki ambacho mvua inaendelea kunyesha nchi nzima.
Aidha ametoa maelekezo kwa wakazi wa kata ya Ikuti na Malindo kusitisha Matumizi ya Barabara ya Tukuyu-Kapugi-Ikuti na badala yake waendelee kutumia barabara ya Kyimo- Iponjola-Ikuti kwa ajili ya shughuli za usafirishaji wa watu na mali zao.
Pia ametahadharisha wakazi wote wanaoishi katika maeneo hatarishi kuchukua tahadhari ili kujiepusha na maafa yanayoweza kujitokeza na hatimae kuchukua uhai wa watu na mali zao.
Mpaka sasa hakuna madhara yaliyojitokeza katika maporomoko haya zaidi ya barabara na Mashamba kumeguka na kujaza matope na miamba katika mto Kiwira.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa