MARALIA SASA BASI
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mheshimiwa Jaffar Haniu leo tarehe 31.10.2023 amezindua zoezi la ugawaji wa vyandarua bure kwa wanafunzi wa shule za Msingi lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa wa maralia kwa kuzuia visumbufu( Mbu) na maambukizo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine
Zoezi hili limezinduliwa katika shule ya msingi Tukuyu na limeratibiwa na Bohari ya Dawa nchini ( MSD).
Uzinduzi umeenda sambamba na Kauli mbiu " Malaria sasa basi"
Mhe.Haniu ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na serikali kupitia Wizara ya afya kuhakikisha afya za wananchi zinalindwa na hivyo kupanua nguvu kazi ya taifa.
Amesema vyandarua hivi vinatolewa bure kwa wanafunzi hivyo asingependa kuona wazazi wanavitumia kinyume na malengo mahususi ikiwemo kuvulia samaki na wigo wa bustani dhidi ya ndege na wanyama wengine.
Mhe. Haniu ameonya watu wanaotoa elimu Potofu kuwa vyandarua hivi vina madhara na kuwa kufanya hivyo kunarudisha nyuma juhudi za serikali kwani vimefanyiwa utafiti na vinafaa kwa matumizi na kinga ya maralia kwa watoto na jamii kwa ujumla.
Aidha amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU pamoja na Police Rungwe (OCD) kuhakikisha wanakamatwa wote watakaojaribu kutorosha Vyandarua kwenda nchi za jirani.
Mfamasia kutoka MSD Bi. Caroline Cornelius ametaja kuwa jumla ya vyandarua 43149 na shule 150 zitanufaika na mpango huu na zoezi linatarajia kuanza mapema kesho
Bi Caroline ameomba Walimu wakuu, kamati za shule pamoja viongozi wa vijiji, kutoa ushirikiano wa kutosha ili zoezi hili likamilike kwa wakati na ufanisi mzuri.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa