MAPATO YA NDANI YALETA "RAHA" KWA WAKAZI WA WILAYA YA RUNGWE
Zaidi ya Shilingi million 62 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Msingi Umoja yenye Mchepuo wa Kingereza iliyopo Ilenge kata ya Kyimo.
Shule hii inatarajia kuanza kutoa huduma ya elimu kuanzia kesho tarehe 5.2.2024 ambapo Fomu za namna ya kujiunga pia zitatolewa
Ujenzi umejumuisha vyumba vya madarasa, ofisi pamoja na vyoo vya walimu na wanafunzi.
Shule hii imeondoa changamoto ya umbali wa kufuata huduma ya elimu katika shule ya Nuru ambayo pia humilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Shule nyingine inayotarajiwa kufunguliwa kesho ni pamoja na Ushirika iliyopo kata ya Mpuguso.
Shule Mpya ya mchepuo wa kiswahili inayotarajiwa kuanza kutoa huduma ya elimu kesho ni Chief Mwanjali iliyopo kata ya Ikuti mita chache kutoka katika Gulio la Ikuti.
Wazazi mnahamasishwa kuwaandikisha watoto katika shule hizi kwa maendeleo endelevu ya taifa letu.
----Endelea kulipa mapato ya serikali kwa ufanisi na maendeleo katika sekta Mbalimbali----
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Renatus Mchau
Msemaji Mkuu wa Serikali
CCM MKOA WA MBEYA
MBEYA YETU (GROUP LA MKOA WA MBEYA)
Atubonekisye Mshani
Ikulu Mawasiliano
MBEYA YETU WOTE
Mbeya Press Club
RUNGWE YETU" Mbeya".
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa