Katika kuboresha huduma ya afya Hospitali ya wilaya ya Tukuyu- Rungwe (Makandana) inaendelea kutumia Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA) katika nyanja Mbalimbali.
Mfumo wa utoaji wa taarifa za mgonjwa na kuzihifadhi (The Government of Tanzania,Hospital Management Information System-GOT-HOMIS umerahisisha utoaji wa huduma kwa haraka hii ikiwa ni pamoja na kutunza kumbukumbu za mgonjwa, Kuratibu mzunguko wa dawa, kuharakisha malipo, uondoaji wa njia ya kutumia karatasi/ faili na badala ya yake maelezo ya mgonjwa, vipimo na matokeo ya vipimo kutumwa kwa njia ya mtandao/ mfumo unaoendeshwa na vifaa maalumu na vya kisasa hospitalini.
Mfumo wa Kamera (CCTV CAMERA) uliopo kona zote za hospitali (Masaa 24) unarahisisha kuratibu matukio yote yanayoendelea katika Hospitali hiyo na hivyo kuleta ufanisi katika utatuzi wa changamoto mbalimbali.
Serikali ya awamu ya sita inaendelea kusambaza dawa katika Hospitali ya Makandana, Vituo vya 4 vya afya ikwa ni pamoja na zahanati zote 42 sambamba na kufanya ukarabati wa majengo na miundombinu yake.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa