Mafunzo ya kampeni maalumu ya uandikishaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano (05) yamezinduliwa leo tarehe 28.06.2021 na Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt Vicent Anney kwa Watendaji wa kata na wahudumu wa afya ambapo imeagizwa kuwa kila mzazi au mlezi kuhakikisha anampeleka mtoto katika ofisi ya kata au kituo cha afya/zahanati iliyokaribu ili kupata huduma hii ambayo inatolewa bure kwa siku tano mfululizo.
Zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe 29.06.2021 siku ya jumanne mpaka siku ya jumamosi tarehe 03.7.2021 huku likihitaji mzazi au mlezi kuleta viambata vifuavyo
1. Kadi ya kliniki
2. Tangazo la kizazi
3. Alifahamu jina mtoto na majina ya wazazi wote wawili ipasavyo
Ikumbukwe kuwa huu ni mpango maalumu na wa kudumu ukilenga kuhakikisha watoto wote wanapata vyeti vya kuzaliwa na cheti hiki kitatumika hata baada ya mtoto kuvuka miaka mitano.
Aidha hiki ni cheti halali kitakachomsaidia mtoto kupata huduma za matibabu, elimu, safari pamoja na ajira.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa