Mafunzo ya kujengeana uelewa kwa wadau mbalimbali juu ya utekelezaji wa kipindi cha pili cha- TASAF- awamu ya tatu yamezinduliwa leo tarehe 10.8.2021 na Mkuu wa wilaya ya Rungwe Dk. Vicent Anney yakilenga kubaini na uandikishaji wa kaya masikini.
Aidha Dk. Anney ameongeza kuwa lemgo la TASAF ni pamoja na Kuwaongezea uwezo wananchi uwezo wa kujiajiri, kuongeza mapato ya kaya na familia kwa ujumla, Kuongeza maarifa na ujuzi ina kuongeza fursa ya jamii katika ujasiriamali.
Hata hivyo ameonya wadau kutoonesha upendeleo wa aina yeyote wakati wa kuzibaini na kuzisajiri kaya masikini.
Jumla ya shilingi tirion 2.03 zinatarajia kuzinufaisha kaya masikini Tanzania bara na Visiwani huku zikiwa na sifa zifuatazo:
1.Kaya zenye uwezo wa kufanya kazi na zenye watoto
2. Kaya zenye uwezo wa kufanya kazi na zisizo na familia.
3. Kaya zenye watu wenye ulemavu
4. Kaya zenye watoto wanaolea/ongoza familia
Wakati huohuo Dk Anney ameagiza miradi yote inayotekelezwa vijijini kutumia kaya masikini kama nguvu kazi ili kuzijengea uwezo kiuchumi na hivyo kuvunja ukuta wa umasikini unaozikabili kwa muda mrefu.
Katika awamu hii imearifiwa kuwa fedha zote zitaingizwa kwenye akaunti za wanufaika kupitia akaunti za benki, simu za mkononi au mawakala maalumu badala ya kupewa mkononi lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kuwafikia walengwa kwa wakati.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa