Shule za sekondari kwa kidato cha sita nchini zinafunguliwa kuanzia tarehe 1 june,2020.
Mwalimu Abel Ntupwa ni afisa elimu Sekondari halmashauri ya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya na ametoa maelekezo yafuatayo.
1. Wanafunzi watatakiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe 30 mwezi mei bila masharti yeyote.
2.Wanafunzi watatakiwa kuepuka misongamano ikiwa ni pamoja na kutoshirikiana vyombo vya chakula, nguo nakadharika.
3. Wanafunzi watatakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara angalau dakika 30 kila siku.
4.kila Shule iandae maeneo ya kunawa hasa madarasani, bwaloni, maabara na bwenini kwa kuweka vitakasa mikono na maji tiririka.
5. Wazazi wasipange ratiba ya kwenda kuwaona wanafunzi shuleni.
6.Endapo mgonjwa atagundulika uongozi wa shule uwasiliane na kituo cha afya kilicho jirani au ofisi ya Mkurugenzi wilaya.
7. Masaa mawili yameongezwa kutoka muda uliozoeleka wa kufundisha wanafunzi darasani ili kufidia muda uliopotea hapo awali.
8. Walimu na Wanafunzi waepuke kuzurura kwani kufanya hivyo wanaweza kuletea maambukizi shuleni.
9 Kila shule iondoe hofu kwa wanafunzi kwa kuwapa ushauri nasihi kila mara inapowezekana.Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ina shule zenye watahiniwa wa kidato cha sita ikiwemo shule ya sekondari Kayuki, Rungwe, Tukuyu, Isongole, God's Bridge, Lubala pamoja na Lutengano.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa