Waheshimiwa Madiwani kutoka kata zote 29 pamoja na viti maalumu na baadhi ya Watalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wamefika salama katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga Leo tarehe 19.9.2022 ikiwa ni sehemu ya Mwaliko kutoka Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Manispaa ya Kahama.
Katika ziara hii fupi Madiwani wanatarajia kujifunza
1. Utaratibu bora wa Matumizi ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji
2. Namna ya kusimamia shughuli za uwekezaji ili kuongeza kipato kwa wananchi na Kodi kwa Halmashauri.
3.Kutumia vikundi vya Halmashauri katika kutekeleza miradi ya Maendeleo ndani ya Halmashauri.
4..Namna jamii inavyonufaika na faida inayotolewa na makampuni baada ya kupata tija katika shughuli zao (Corporate social Responsibility).
5. Ukusanyaji wa ushuru wa huduma kutoka kwa WAFANYABIASHARA.
Ndani ya ukumbi wa
Manispaa ya Kahama Mchumi wa Manispaa ameeleza kuwa jumla ya maeneo sita yametengwa kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.
Katika eneo la Viwanda la Ummy Mwalimu lililopo takribani Km 3.4 kutoka Mjini Kahama Barabara ya Tinde- Isaka- Burundi lenye ukubwa wa ekari 500 ndilo eneo pekee lililokusanya wajasriamali kutoka Mjini kama karakana za kuchomelea, Viwanda vidogovidogo vya kuchakata bidhaa za kilimo na mifugo, Mafundi seremala na mpaka Sasa eneo hili limechangia asilimia 10% ya mapato ya ndani.
Mpaka Sasa wajasriamali wote wameondolewa mjini na wamepelekwa katika eneo hili na tija kubwa imeanza kuonekana.
Moja ya tija ni urasimishaji wa shughuli za kiuchumi zinazopatikana katika eneo hili, na utoaji wa leseni za biashara imekuwa rahisi ambapo imesaidia upatikanaji wa Mikopo kwa urahisi kupitia asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri na mikopo mingine kutoka taasisi za kifedha.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa