Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wamechangia jumla ya sh 585,000/= kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kayuki.
Akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 31/10/2018 katika Ukumbi wa Halmashauri, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Ezekiel Mwakota alisema Madiwani hao walikubaliana kuchangia fedha hizo ili kuendeleza ujenzi wa shule hiyo.
Mhe. Ezekiel Mwakota alisema, awali Serikali Kuu ilitoa Sh.milioni 252 kwa ajili ya ujenzi huo ambazo hazikuweza kukamilisha ujenzi hivyo shule iliandaa harambee mbalimbali na kuomba michango kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta ya elimu. Jumla ya shilingi 51,156,700/= ziliipatikana katika harambee iliyo ratibiwa na Naibu Sika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DR. Tulia Ackson. Ambapo ahadi ilikuwa ni sh.27,312,000/= na taslimu ilikuwa 3,844,700/=.na milioni 1 iliahidiwa kutolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya usanifu wa miundo mbinu ya maji.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ezekiel Mwakota aliwashukuru sana wadau mbalimbali wa sekta ya elimu ambao wanachangia katika kuendeleza na kuinua elimu wilayani Rungwe, mfano,Tulia Trust Fund kwa kusaidia ujenzi katika shule za Sekondari Kayuki, Bulyaga na Masoko. Aliagiza wadau hao waandikiwe barua za shukrani na uthamini wa michango hiyo.
Katika Mkutano huo wa Baraza la Madiwani Mwenyekiti wa Halamshauri alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya Bi.Loema Peter kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ya Halmashauri kwa mwaka wa 2017/2018 kwa kuvuka lengo kwa kukusanya 86%.
Pia aliwataka kuongeza juhudi katika ukusanyi wa mapato ambao umefika 19% na kuwa nyuma asilimia 6 kufikia lengo la 25% kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019. “Hivyo ni vyema kuongeza juhudi ilikufika lengo hilo lilokusudiwa” alisema Mhe. Ezekiel Mwakota. Vilevile alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kutekeleza jukumu la kubuni miradi ya kimkakati kwa Wilaya yetu kwa kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani ambayo itafanya Halmashauri iweze kujiendesha na kuwa na mapato endelevu. Licha ya kwamba tayari Halmashauri imekwishapeleka miradi ya kimkakati wizarani yenye ujenzi wa vibanda vya biashara katika eneo la Stendi ya vumbi Tukuyu Mjini yenye thamani ya shilingi milioni 578, lakini bado mradi huo unathamani ndogo hivyo ni vema kuandaa Miradi ya kimkakati yenye thamani kubwa na yenye tija. Pia alishauri kufanya ufuatiliaji mzuri katika kiasi hicho kidogo kinachopatikana.
Katika Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe Bi.Loema Peter aliwaomba waheshimiwa Madiwani wawe na umoja na ushirikiano juu ya ukusaji wa mapato ya Halmashauri amesema “katika ukusanyaji wa mapato wakati mwingine nguvu hutumika. Na nikiziweka nguvu hizo, kilio kitasikika. Mkisikia kilio huko naomba mtulie naniombe tu; mmenisisitiza nikakusanye, naomba Mhe. Mwenyekiti mnipe ushirikiano, tushirikiane katika kukusanya na mniunge mkono”. Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri alikubaliana na kauli hizo na kuwaomba waheshimiwa madiwani kutoa ushirikiano katika suala la ukusanyaji wa mapato.
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, iliwekewa lengo la kukusanya billion 3.9 na ilifanikiwa kufikia 86% ya makusanyo yake na sasa imepangiwa kukusanya bilioni 5.2 kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Katika robo hii imefikia asilimia 19 ya makusanyo yote.
Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa