Ziara ya Waheshimiwa Madiwani kutoka Manispaa ya Iringa katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imehitimishwa leo tarehe 20.5.2023 kwa kutembelea Shamba la Mfano la Migomba lililopo katika kijiji cha Kalalo kata ya Lufingo, Kiwanda cha Gesi (TOL GAS) na Shule ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu Katumba.
Katika shamba la Mkulima katika kijiji cha Kalalo Madiwani wamejifunza kilimo cha tija ambapo Mkulima hujishughulisha pia na Ufugaji.
Bwana Juma Mwakifulefule ndiye aliyetembelewa ambapo ameeleza kuwa katika shamba lake la ekari saba kila mwezi huvuna mikungu 100 na kujipatia kiasi cha Shilingi
Million 2 na kila miungu huuzwa kwa wastani wa shilingi 20,000/=
Aidha Samadi ya Ng'ombe hutumika kurutubisha shamba la Migomba na kwa idadi ya mifugo yake huzalisha lita 200 kwa siku sawa na wastani wa pato la shilingi 140,000/ = kwa siku.
Katika kiwanda cha gesi wamejifunza namna gesi inavyozalishwa na kuuzwa katika viwanda vya kusindika vinywaji ndani na nje ya nchi.
Gesi hii husambazwa katika viwanda vyote vya Pombe na soda katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mbeya, Dar, Kilimanjaro Morogoro na nchi za Zambia, Kenya na Zimbabwe.
Wakiwa katika shule ya Msingi Katumba II wamefarijika na huduma ya elimu inayotolewa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu huku kiwanda cha ASAS kikitoa kiasi cha lita 50 za maziwa bure kwa siku kwa ajili ya kuboresha lishe ya Wanafunzi.
Madiwani wamekabidhi zawadi kadhaa ikiwemo mifuko ya sukari, Mchele, Vinywaji, na mafuta ya kupikia.
Aidha wamekabidhi zaidi ya shilingi laki 2 kama motisha kwa wanafunzi na walimu.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa