Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imeanza maandalizi ya kwa kupitia na kujadili rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Aidha katika kikao hicho cha kujadili rasimu hiyo pia ilijadiliwa mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa bajeti ya Halmashauri Mwaka wa fedha 2018/2019. Katika mafanikio ya utekelezaji wa bajeti hiyo Halmashauri ilipata mafanikio ya kitaaluma kwa kuongezeka kwa ufaulu kwa matokeo ya mitihani ya darasa la saba kutoka 68.7% mwaka 2017 hadi kufikia 87.4% mwaka 2019, kuwezesha wanafunzi 5,408 waliofaulu darasa la saba 2018 kuingia kidato cha kwanza 2019.
Katika matokeo ya mitihani ya kumaliza kidato cha Nne mwaka 2017,Halmashauri ilishika nafasi ya tatu kimkoa kwa kufaulisha kwa80% na katika matokeo ya kidato cha sita Halmashauri ilifaulisha kwa 99.3%.
Halmashauri ilifanikiwa kuongeza kiwango cha utoaji mikopo kwa vikundi vikundi vya Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kutoka tsh 156,070,000.00 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi kufikia tsh 349,900,000.00 kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Aidha Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanikiwa kuongeza viwanda ambavyo vimesaidia jamii kupata ajira ,viwanda vilivyo ongezeka ni kiwanda cha maji ya kunywa "Tukuyu Springs Water" kiwanda cha maziwa ASA na kiwanda cha parachichi Rungwe Avocardo co.
Halmashauri imefanikiwa katika kupunguza kwa maambukizi ya VVU/UKIMWI toka 9.2% 2017/2018 hadi kufikia 9% 2018/2019.
Kwa upande wa mifugo koosafu za ng'ombe wa maziwa zimeboreshwa kwa 82% .
Kwa kuboresha huduma za afya Halmashauri imekamilisha ujenzi wa vituo vya afya 3 vya Ikuti,Isongole na Masukulu vimekamilika na kuanza kutoka huduma.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa