MAADHIMISHO YA SIKU YA LISHE KITAIFA 24 hadi 30 Oktoba 2024.
Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imeanza maadhimisho ya wiki ya Lishe Duniani katika kata zote 29.
Kauli mbiu Mwaka huu ni "*Mchongo ni Afya yako, Zingatia unachokula"*
Kauli mbiu inahimiza jamii kuchukua hatua makusudi ya kuwa makini na kufanya maamuzi sahihi kuhusu aina na ubora wa vyakula wanavyokula au kuwalisha watoto, ili kulinda afya zao kwa ustawi kamili kijamii na kiuchumi.
Lengo la Maadhimisho haya Ni kutoa elimu ya Lishe kwa jamii kwa kuzingatia mapendekezo ya mwongozo wa kitaifa wa chakula na ulaji
MALENGO MENGINE MAHUSUSI
-Kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya vyakula vilivyoongezwa virutubishi
-kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni za ulaji unaofaa"*kula mlo kamili"* ili kukidhi mahitaji yote ya kilishe ya mwili na kuwa na afya bora.
-Kupambana dhidi ya uelewa duni, dhana potofu na mitazamo hasi iliyopo katika jamii husika kuhusu masuala ya Lishe kwa kutoa taarifa sahihi na za kitaalam
-Kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi na kushughulisha mwili ili kupambana dhidi ya utapiamlo wa Lishe ya kuzidi hivyo kuepuka magonjwa yasiyoambukiza yenye uhusiano wa Lishe kama vile kisukari, saratani, magonjwa ya moyo
-Kuunganisha jamii na wadau mbalimbali katika kuendeleza juhudi mbalimbali zinazolenga kuimarusha afya ya jamii.
Maadhimisho ya Siku ya Lishe kwa mwaka 2024 yatafanyika katika mikoa na Halmashauri zote Tanzania bara kama ambavyo imekuwa ikifanyika kila mwaka. Mkoa wa Dodoma umeteuliwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya Kitaifa.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa