Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yamefanyika leo tarehe 8/03/2021 ambapo katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe yameadhimishwa katika ukumbi wa halmashauri - Mwankenja.
Mheshimiwa Lydia Sanga diwani wa Kata ya Ibigi ndiye alikuwa mgeni rasmi na amewaomba Wanawake kuendelea kuibua fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzitumia huku wakipinga vitendo vya kikatili vinavyoendea katika maeneo yao na kuficha nyuma fursa za maendeleo miongoni mwao.
Aidha amewahamasisha Wanawake kuendelea kuchangia chakula mashuleni ili kuongeza ufaulu sanjari na kutokomeza utapiamlo na udumavu Kwa wanafunzi.
"Mama ana jukumu la kuhakikisha mtoto amekula na ameshiba, ni aibu kuona mwanao anaenda shule huku akishinda kutwa nzima bila kula chochote" amesisitiza. " Tuwaache waalimu wafundishe watoto wetu na sisi kazi yetu iwe ni kuzihamasisha Kaya zetu kuchangia chakula shuleni"" ameongeza huku akishangiliwa na mamia ya Wanawake waliohudhuria maadhimisho hayo.
Katika maadhimisho hayo zaidi ya shilingi laki TATU zimekusanywa ikiwa ni juhudi za kuwahamasisha Wanawake wa Kata ya Ikuti kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF).
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa