Maadhimisho ya siku ya elimu yamefanyika leo tarehe 3.7.2024 katika Ukumbi wa land mark Tukuyu Mjini wilayani Rungwe lengo likiwa ni kupongezana na kukumbushana majukumu mbalimbali ya utoaji wa elimu katika shule za Msingi na Sekondari.
Maadhimisho haya yamekuja huku ufaulu ukizidi kupaa juu ambapo mwaka 2023 ufaulu Mtihani wa Kuhitimu elimu ya Msingi ulikuwa asilimia 94.7% na Sekondari kidato cha pili 90.5% nne 95.9 % na kidato cha sita 99%
Shule zilizofanya vizuri kwa upande wa Msingi ni pamoja na Kiwira, God's Bridge, Goje, Bagamoyo, Magereza, Kells, na Nuru.
Kwa Upande wa Sekondari ni Rungwe, Kayuki, Bulyaga, Tukuyu, Lubala, Gods Bridge Joy Girls, na St Almano
Katika maadhimisho haya zawadi mbalimbali zimetolewa kwa walimu, wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu.
Zawadi hizo ni pamoja na vyeti, Fedha taslimu na ngao.
Makundi yaliyopata zawadi ni wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao, Walimu waliofaulisha vema katika masomo yao, shule bora katika utunzaji wa mazingira, na wadau waliochangia ufanikishaji wa siku hii muhimu.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa