LISHE BORA KWA MAISHA YETU
Noah kibona, Rungwe Dc
Imeelezwa kuwa uzingatiaji sahihi wa lishe katika ngazi ya kaya huchochea ustawi bora wa jamii ukiwemo ukuaji wa ubongo na afya ya mwili.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Rungwe Bibi Loema Peter wakati akiongea na wadau wa Lishe Ofisini Kwake ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza jamii kuzingatia chakula chenye viini lishe.
“Inashangaza kuona watoto wanapata Udumavu na Utapiamlo ili hali wilaya ya Rungwe inazalisha vyakula vya aina mbalimbali” aliongeza Bi. Loema. Kutotilia mkazo katika kilimo, ufugaji mazoea wa wanyama na mazao ya nyuki kumechangia baadhi ya familia kukumbwa na magongwa nyemelezi yatokanayo na ukosefu wa lishe.
Wilaya ya Rungwe inayopatikana katika latitude 9 o 00 ′ na 9 o 30 ′ E na longitude 33 o , 34 o S na eneo la mraba, kilometa zipatazo 2 221 lenye mwinuko wa 770 m a.s.l to 2 265 m a.s.l, inaiwezesha wilaya hii kupata mvua nyingi zinazochochea kulima mazao ya mizizi kama karanga, viazi vitamu na mviringo, magimbi na njugu. Matunda kama ndizi, mananasi na maparachichi hupatikana kwa wingi pia. Mahindi, mpunga na mihogo pia yanastawi kona mbalimbali. Mazao haya yakilimwa kwa wingi kwa kufuata ushauri wa mafisa ugani tatizo la utapiamlo linaweza kumalizika kabisa.
UZALISHAJI WA MAZIWA
Wakazi wa Wilaya ya Rungwe wanafuga mifugo mbalimbali. Ng’ombe wanafugwa takribani kila kaya. Afisa mifugo na Uvuvi wilaya ya Rungwe Dr. Lawrance Kibona anabainisha kuwa wastani wa lita milioni 44 huzalishwa kila mwaka. Sawa na lita 140,000 kwa siku. Kila kaya hutumia lita mbili kama chakula na mengine huyauza kwa lengo la kukuza kipato cha kaya. Dr Kibona anafafanua kuwa kwa wastani kila kaya ina wakazi wanne hivyo kila mkazi hutumia nusu lita kwa siku na hivyo kujinasua na lindi la utapiamlo na udumavu kwa watoto hasa walio chini ya miaka miwili.
HALI YA LISHE KATIKA MKOA WA MBEYA
Hata hivyo akitoa takwimu za hali ya Lishe katika mkoa wa Mbeya katika kikao cha Afua za Lishe kilichofanyika mwezi desemba mwaka jana, Afisa lishe mkoa wa Mbeya bwana Benson Sanga alisema kuwa kwa sasa udumavu kimkoa umepungua ambapo mwaka 1991 ulikadiriwa kufikia asilimia 50 na mwaka 2018 umepungua kufikia asilimia 32 hali inayotia moyo na kupunguza tishio la kupata watoto wenye uwezo mdogo wa kufikiri, kukosa umakini na zaidi akina mama kupata shida wakati ya kujifungua na kupata watoto wenye ulemavu akitolea mfano ugonjwa wa mgongo wazi na vichwa vikubwa.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa