KYIMO ENEO LA KIMKAKATI WILAYANI RUNGWE
Kyimo -K.K.K (Kyimo Kijiji Kitulivu), Makao makuu ya kata inayokuwa kwa kasi huku ikiwa na eneo maalum lililotengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya shughuli za uwekezaji wa viwanda, afya na elimu pamoja na ofisi za umma.
Serikali imesogeza miundombinu ya maji, barabara, na umeme ili kutoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza mitaji yao kwa ufanisi.
Katika eneo hili tayari kuna jumla ya viwanda vinne vimejengwa kikiwemo kiwanda cha Maziwa ASAS DIARIES, KUZA, KORONGO TATU na LIMA Ltd, RUNGWE SPRING WATER na TUKUYU.Kiwanda kingine cha usindikaji wa wa maji na Matunda kipo mbioni kujengwa.
Viwanda vyote hivi vinapatikana kata ya Kyimo eneo maalum la uwekezaji.
Hatua ya ujenzi wa viwanda hivi imeongeza ajira kwa Wakazi wa Wilaya ya Rungwe na kuvutia ujenzi na utoaji wa huduma mbalimbali kama elimu ambapo jumla ya shule tatu za mchepuo wa kiingereza zimejengwa katika eneo hili huku vyuo viwili kikiwemo kituo cha mafunzo ya stadi za kilimo kikiendelea kuleta ufanisi kwa wakulima.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa