Kiwanda cha Maji Tukuyu kimezinduliwa leo mapema na Waziri wa uwekezaji Mhe. Angela Kairuki katika kijiji cha Kibisi kata ya Kyimo wilayani Rungwe.Akizundua kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya Majinja Logistic, Mhe. Kairuki ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kuendelea kuandaa mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji kwani kwa muda mfupi kimesaidia upatikanaji wa ajira zaidi ya 1000.
Kiwanda hicho ambacho ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi Billion moja kimesaidia upatikanaji wa maji safi kwa zaidi ya kaya 50, ujenzi wa barabara kwa umbali wa kilometa 1.8, kimetoa bati 100 na mifuko ya saruji 100 kwa shule ya Msingi Kibisi, na kimeahidi kusambaza umeme kwa kaya zote zinazozunguka kiwanda hicho.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa