Mamia ya wakazi wa kata ya Kyimo wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kituo cha afya Kyimo.
Uzinduzi umeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe.Mpogigwa Mwankuga.
Uzinduzi umehusisha pia viongozi wa kidini, Machifu, Vyama vya kisiasa pamoja vikundi vya burudani.
Akizindua kituo hiki Mhe.Mwankuga ameeleza kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi Million 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki hii ikihusisha pia ujenzi wa nyumba ya watumishi wa afya ambayo imegharimu kiasi cha shilingi million 90
Pamoja na hayo amewakumbusha wakazi wa kata ya Kyimo kujiunga na Bima iliyoboreshwa ikiwa ni nyenzo muhimu ya kupata huduma bora na kwa ufanisi zaidi.
Aidha amewasisitiza wakazi wa kata hii na Rungwe kwa ujumla kujitokeza na kupima afya zao ili kujijengea maisha endelevu na Uzalishaji mali.
Zaidi ya Wagonjwa 60 wamejitokeza na kupima afya zao sambamba na kupata matibabu mbalimbali ikiwemo huduma ya chanjo pamoja matibabu ya watoto.
Pamoja hayo Mkurugenzi Mtendaji Halimashauri ya wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau ameeleza kuwa serikali imeendelea na ujenzi wa vituo mbalimbali Wilayani Rungwe ikiwemo kituo cha Afya Ndanto, Iponjola, Kinyala na Kiwira pamoja na jengo la wagonjwa wa nje ghorofa moja katika hospitali ya wilaya Tukuyu kwa zaidi ya shilingi Billion 2.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa