Shule ya sekondari Kisondela imefuzu ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu 14 ya vyoo .
Shule hii yenye jumla ya wanafunzi 659 na walimu 30 inatarajiwa kuongeza kiwango cha ufaulu baada ya miundo mbinu ya kusoma na kujifunzia sasa kukamilika ikiwemo Maabara, Maktaba, umeme, maji, vyumba vya madarasa, walimu wa kutosha, na chakula shuleni.
Mbele ya kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango (FUM), Mkuu wa Shule hiyo Mwal. Theresia Mgimba ameeleza kuwa ujenzi wa vyumba hivyo umegharimu zaidi ya shilingi Million 45 hii ikijumuisha mchango wa serikali na nguvu za wananchi.
Kamati imepongeza kazi nzuri iliyofanyika huku wakiomba uongozi wa shule hiyo pamoja na wananchi kuendelea kutunza miundombinu hiyo ili ivinufaishe vizazi vijavyo.
MAZINGIRA YA SHULEUongozi wa shule kwa kushirikiana na Wanafunzi wamepanda miti ya kutosha kwa ajili ya Mbao, matunda na kivuli yakiwemo maua hali inayochochea wanafunzi kusoma kwa bidii.
SHULE YA KISONDELA INAVYOZUNGUKWA NA VIVUTIO VYA KITALII.
Kando ya shule hii kuna kambi ya zamani ya wagonjwa wa ukoma pamoja na kanisa kongwe zaidi ambalo lilitumika kuabudia ikwa ni sehemu ya kuwatenga na kupunguza maambukizi. Majengo haya kwa sasa yamebaki kama sehemu ya historia na baadhi yakitumika kutolea huduma ya afya (zahanati ya Makete).
Aidha kuna misheni ya Kanisa la katoliki (Kisa) na Lutengano (Moravian) ambazo zimebeba amali za kale na historia ya kuenea kwa dini ya kikiristo katika ukanda huu.
Kijiji cha matofali ambalo ndiyo eneo pekee linalozalisha matofali ya kuchoma hata msimu wa mvua limekuwa kivutio tosha kwa wageni.
Maporomoko ya maji Kaporogwe yanampa nafasi mgeni kuona mwanguko wa maji unavyo vuta hisia katika eneo hili.
MTANDAO WA BARABARA YA LAMI.
Barabara ya lami kutoka Masebe - Mpuguso TTC- Bugoba na ile ya Masebe - Lutete imerahisisha usafiri wa wanafunzi na walimu na hivyo kuwa na wakati mzuri wa kuandaa masomo kwa wakati na ufanisi mzuri.
UZALISHAJI MALI NA UWEKEZAJI KATIKA UKANDA HUU
Eneo hili linafaa kwa uwekezaji wa kilimo cha Kahawa, Parachichi, Migomba, miti ya mbao, tangawizi.
Ujenzi wa hoteli na kambi za kitalii hasa maeneo ya vivutio.
Uwekezaji wa viwanda na maeneo ya kutolea elimu ya Msingi, sekondari , vyuo na ufundi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa