Karibu Kisa kata ya Kisondela eneo lililobeba historia mwanana ya ujio wa Wamisionari katika wilaya ya Rungwe na ujenzi wa kituo cha kulelea wagonjwa wa Ukoma.
Eneo hili lenye ekari kadhaa lilitumika kuhufadhia watu walioshukiwa na kukutwa na ugonjwa ukoma ikiwa ni sehemu muhimu ya kuwahifadhi, kupata matibabu na hivyo kuzuia maambuki kwa watu wengi zaidi.
Eneo hili lililopo kilometa kadhaa kutoka Chuo cha Ualimu Mpuguso sasa linafikika kwa barabara ya lami Masebe-Lugoba.Ukifika utastajabishwa na ufundi wa majengo ya kale yalivyosanifiwa na kudumu kwa muda mrefu na hivyo kuwa kivutio kwa watalii.
Wagonjwa wa Ukoma walijengewa kanisa lao ikiwa ni hatua ya kuwatenga sambamba na kupata neno la kiroho kutoka kwa viongozi wa Kidini hasa kanisa la Katoliki na Moraviani.
Kwa sasa wagojwa hao hawapo tena na majengo yake yanatumika kwa ajili ya ibada ya kikiristo, zahanati ya serikali- makete na mengine hutumika kama majengo ya utawala kwa shule ya sekondari Kisondela.
Vivutio vingine katika eneo hili ni pamoja maporomoko ya maji Kaporogwe, Kisa misheni (katoliki), Lutengano misheni (Moraviani) na Kaburi la mzungu wa kale zaidi katika kijiji cha Kapugi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa