Katika Msimu wa 2021/22 halmashauri ya wilaya ya Rungwe inatarajia kupanda miche ya kahawa zaidi ya million 2.4 huku miche 163,000 ikitolewa na taasisi ya utafiti wa kahawa- TACRI. Miche hii itasambazwa katika vijiji mbalimbali vinavyozalisha zao la kahawa.
Felician Urio ni ukaguzi wa kahawa wilaya ya Rungwe na amewaomba wakulima kuanza kupanda zao hili mapema ingali mvua zinanyesha huku wakitumia mbolea ili kurutubisha udongo ikiwa ni pamoja na kunyunyizia viwatilifu Kwa lengo la kuangamiza visumbufu vya mimea.
Bei ya kahawa kwa kilo msimu uliopita ilikuwa Kati ya shilingi 4000 /= hadi 5610/= kulingana bei ya soko hali iliyoinua kipato Kwa ngazi ya kaya na taifa Kwa ujumla huku wakulima wilaya ya Rungwe wakijenga nyumba bora, kusomesha watoto, mitaji ya biashara, na kulipia bili mbalimbali.
Katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe zao la kahawa huongozwa na kulimwa zaidi katika kata zifuatazo:
1. Ikuti
2.Mpuguso
3.Nkunga
4.Kisondela
5.Bujela
6.Lufingo7
.Lupepo
8.Malindo
9. Iponjola
10. Ilima
Kahawa iliyokaushwa na kuandaliwa vizuri hutumika kama :- kinywaji Kwa kuchanganya na sukari au tupu- Kutengezea madawa-Kuongeza radha kwenye vinywaji baridi na pombe Kali.
Mnada wa zao la kahawa katika Mkoa wa Mbeya na Songwe hufanyika katika Mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa