Wakuu wa shule za sekondari wafanya kikao kazi cha kwanza kwa mwaka 2019, ni ada kwa Idara ya elimu sekondari kufanya vikao na wakuu wa shule ili kuwa kumbusha wajibu wao katika utendaji wa kazi na kuweka mipango mikakati kwaajili ya ufaulu
Wakuu wa shule za sekondari wafanya kikao kazi cha kwanza kwa mwaka 2019, ni ada kwa Idara ya elimu sekondari kufanya vikao na wakuu wa shule ili kuwa kumbusha wajibu wao katika utendaji wa kazi na kuweka mipango mikakati kwa ajili ya ufaulu mzuri katika shule zote. Kikao hicho kimefanyika tarehe 10/01/2019 katika ukumbi wa kituo cha walimu kilichopo Tukuyu mjini na kuhudhuriwa na Wakuu wa shule 38.
Aidha katika kikao hicho walijadili sheria mbalimbali za utumishi wa umma ambazo ni muongozo katika majukumu yao, sheria na nidhamu kwa walimu na haki za kiutumishi, taratibu za kufuata/miongozo ya matumizi ya fedha za umma, maelekezo ya shughuli za taaluma, na tathmini ya matokeo ya kidato cha Pili 2018. Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi kutoka katika Idara ya elimu sekondari ambao walitoa mada mbalimbali katika kiako hicho na kujadiliwa kwa pamoja viongozi hao na Wakuu wa shule. Bi Mary Stelli Mwinuka ambaye ni Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu katika Halmashauri ya Wilaya Rungwe aliwasisitiza wakuu wa shule kusimamia walimu katika shule zao kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi na kupata ufaulu mzuri ikiwa pamoja na kufuatilia kwa ukaribu masuala ya nidhamu.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa