KIKAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Imearifiwa kuwa viongozi wa dini wakitumia vizuri majukwaa yao kuelekea Uchaguzi mkuu itasaidia Watanzania kuwapata viongozi bora na wenye kuleta maendeleo nchini.
Rai hiyo imetolewa na Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Rungwe bibi Husna Tonni wakati akifungua kikao cha viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu octoba mwaka huu.
Aidha bibi Husna amewakumbusha viongozi hao kuhakikisha maeneo yao hayatumiki kama majukwaa ya kampeni kwani kwa kufanya hivyo itachochea vurugu na kuondoa mshikamano miongoni mwao.
Shehe Hashimu Maseta ni kiongozi wa msikiti wa Tukuyu mjini na amearifu kuwa uwingi wa watu siku ya kampeni si kigezo cha kupata kura nyingi bali nafasi hii inampa nafasi mpiga kura kubaini nani ana sera nzuri za kuleta maendeleo. " maamuzi ya mpiga kura yasichochee vurugu baada ya mshindi kutangazwa kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki wengi" alionya.
Hata hivyo kamanda wa polisi wilaya ya Rungwe OCD- Christina Msyani amewaomba wakazi wa wilaya ya Rungwe kuendelea kudumisha amani na utulivu ili kuwapa nafasi wapiga kura kwapata viongozi wanaowataka kwa kuepuka mihemuko isiyo ya msingi na yenye sura ya kuchochea vurugu.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa