Katibu Tawala Wilaya ya Rungwe Bwana Ally Said Kiumwa amewakumbusha Wazazi kuendelea kuchangia chakula cha Mchana kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ikiwa ni mbinu sahihi ya kuondoa udumavu na Utapiamlo sambamba na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi
Hayo ameyaeleza wakati wa kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kilichoketi leo mapema tarehe 13.3.2024 katika ukumbi wa Halmashauri Mwankeja.
Amesema adhima ya Serikali ni kuhakikisha watu wake wanapata lishe bora ili kuwangea afya bora hatua itakayosaidia kujihusisha katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.
Hivyo kama watoto watapata Lishe bora ni wazi Taifa litakuwa na watu wenye uelewa mzuri wa kutumia rasilimali zinazowazunguka.
Tathmini hii ambayo pia hujumuisha watendaji wa kata , imeagizwa kuwa kila mzazi ahakikishe kwa ngazi ya kaya anazalisha chakula chenye tija kwa afya ya binadamu, kusimamia unyonyeshaji kwa watoto na kuwachukulia hatua wazazi wote wanaokaidi uchangiaji wa chakula cha Mchana kwa wanafunzi.
Mpaka sasa shule nyingi zimeanza kutoa chakula kwa asilimia 100% Mkazo ukiwa ni kuhakikisha zoezi hili linakuwa endelevu.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa