Kikao cha baraza la kazi kimefanyika leo katika ukumbi wa chuo cha Ualimu Tukuyu kikiwakutanisha Waheshimiwa madiwani, Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Rungwe pamoja na watendaji wa kata zote zilizopo katika halmashauri hiyo.
Kikao kilianza kwa wajumbe wote kunawa kwa sabuni na maji tiririka na kisha wajumbe waliketi kwa umbali wa zaidi ya mita moja ikiwa ni juhudi za kupambana na maambukizi ya COVID 19- CORONA.
Katika kikao hicho mengi yalijadiliwa lakini kubwa zaidi ilikuwa ni kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Rungwe ambapo ilitajwa kuwa mapato yamekuwa yakipanda kutokana na juhudi kubwa za watendaji wa serkali.
Akishukuru hatua hiyo diwani wa kata ya Isongole mh. Laurance Mfwango (CCM) aliwashukuru watendaji wa serikali kwa juhudi zao kubwa ambazo wamekuwa wakizielekeza katika kukusanya mapato ya serikali.
Hata hivyo mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Rungwe Mhe. Ezekiel Mwakota aliiomba kata ya Matwebe iliyopo tarafa ya Pakati kuendelea kuboresha mapato yake kwa kusimamia vyanzo vyake kwani kwa muda mrefu Imekuwa nyuma katika kukusanya mapato.
Pamoja na hayo mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter aliwaomba madiwani kuendelea kuwasimamia watendaji waliopo katika meneo yao kuhakikisha wanakusanya mapato pamoja na utawala bora kwani walio wengi wamekuwa wazembe na hivyo kupunguza kasi ya halmashauri kuwahudumia wananchi kwa kukosa fedha.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa