Ukiwa Nzunda kata ya Ndanto utaona mengi ya kufurahisha.
Kijiji hiki kipo katikati ya kijiji cha Swaya na Ntokela Tarafa ya Ukukwe Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.Kijiji hiki ni nyota inayowaka na kuangaza mafanikio makubwa ambayo ni mfano wa kuigwa nchi nzima.
Kwa kutumia mapato yake ya ndani kijiji kinatarajia kujenga soko la kisasa litakalogharimu kiasi cha shilingi million 100 lenye vyumba 78 vya maduka na vizimba 50 ambapo soko hilo litaleta tija ya shilingi million 25 Fedha ambazo zitatumika katika ujenzi wa Nyumba za walimu pamoja na wahudumu wa afya.
Kijiji hiki chenye jumla ya wakazi 2601 kiliasisiwa mwaka 2014 kikimegwa kutoka katika kijiji cha Ntokela na kimefanikiwa kujenga ofisi ya kisasa ya kijiji, shule ya msingi pamoja na zahanati, Miradi yote ikitegemea MAPATO yao ya ndani.
Mathalani kwa Msimu wa 2020/2021 kijiji kimejenga mfumo wa maji uliogharimu kiasi cha shilingi million 103 huku RAWASA wakiunga mkono kwa kuchangia million 13.
Sasa maji yanapatikana katika kaya zoteUchumi wa kijiji hiki hutegemea kilimo cha viazi mviringo na mahindi ambapo kwa kutumia mashamba ya kijiji hujipatia kiasi cha shilingi million 70 Fedha inayopatikana kutokana na kukodisha mashamba ambapo hekari moja hukodishwa mpaka kufikia million 2 na kijiji kina jumla ya hekari 48 za kilimo.
Vyanzo vingine vya MAPATO ni pamoja na asilimia 20 zinatoka Halmashauri kutoka na makusanyo ya ushuru wa mazao, mikataba ya kijiji, nguvu kazi za wananchi pamoja na wadau.Mapato yamesaidia ujenzi wa ofisi ya kijiji ,( million 38), Shule ya msingi (( madarasa 10), Zahanati (million 32), miradi wa maji ( million 103).
Mtendaji wa kijiji hicho bwana Paul Mwanantunzi ameishukuru serikali kwa kuimarisha shughuli za utawala bora katika kijiji huicho kwani ndiyo chachu ya wananchi kujitolea kwa bidii , kusomewa MAPATO na matumizi sambamba na kuona matokeo ya Fedha za kijiji.
Katika mwaka huu wa fedha 2022/23 Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) inatarajia kuimarisha barabara kutoka kijijini hapo hadi kijiji cha Swaya, Barabara ambayo ni kiungo muhimu kwa wakulima wa viazi kati ya kata ya Swaya na NdantoAidha bwana Tito Mpandila mdau na mkulima wa kijiji hicho amesema kuwa ushirikiano kutoka uongozi wa kijiji umesaidia wananchi kujitolea kwani yeye baada ya kuona kazi nzuri alitumia gharama zake kwenda jijini Dar es salaam kununua mabati yaliyotumika kuezekea soko hilo la kijiji
Serikali katika kuunga mkono jitihada za wananchi imejenga kituo cha afya katika kata ya Ndanto mita chache kutoka katika kijiji hicho kwa gharama ya shilingi million 250. Pia ujenzi wa vyuma sita vya madarasa vikiwemo vya mpango wa EP4R na COVID 19 (million 120) katika shule ya sekondari Ndanto pamoja na maabara kwa gharama ya shilingi million 30
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa