Noah kibona, Rungwe Dc
Imeelezwa kuwa kaya masikini zinaweza kuondokana na kazia ya ugumu wa maisha iwapo zitabuni miradi endelevu na inayotekelezeka ili kujinasua katika lindi la umasikini unaozikabili.
Hayo yamesemwa na afisa miradi wa Ujana salama (Cash plus), TASAF Makao makuu bibi Ester Kihuyo wakati akiwasilisha maada ya ubunifu wa miradi wenye kaleta tija na maendeleo kwa vijana wanaoishi katika kaya masikini.
Aidha bi. Kihuyo amesema kuwa miradi mingi katika kaya masikini imekuwa ikizororota kutokana na maafisa ugani kutoitembelea mara kwa mara ili kuijengea uwezo kwa kuitolea ushauri na maelekezo sahihi yenye kuifungulia milango ya mafanikio.
Hata hivyo bi. Kihuyo amesema kuwa mradi wa Ujana Salama unaanda mkakati mahususi wa kuvipa vikundi vya ujasiriamali ruzuku pamoja na kutoa stadi za msingi za uzalishaji mali ili kuvifanya vikundi hivyo kuwa endelevu na vya kudumu katika nyanja za kilimo ,ufugaji na biashara.
Akifungua semina hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter amewataka vijana wote kuhakikisha vikundi wanavyoviunda vinawajengea uwezo wa kujipatia maarifa ya kuongeza kipato ikiwa ni pamoja na kuepukana na maambukuzi ya UKIMWI kwani kwa kutofanya hivyo vikundi hivyo vitakufa na malengo ya mradi yatapotea.
Akitoa muainisho wa vikundi vilivyo pata ruzuku na kuanza kufaidika na matunda ya mradi wa cash plus wilayani Rungwe, mratibu wa shirika la umoja wa mataifa linalo hudumia vijana na watoto (UNICEF) Dr. Frank Etama amesema jumla ya vijana 856 wameshanufaika na elimu ya afya na ujasiriamali pamoja na mbinu za kuweka akiba kwa ngazi ya kaya ili kuboresha maisha kwa kila kaya.
Pamoja na hayo wanufaika wa mradi huo wamehamasishwa kuanzisha miradi kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira ili kupunguza athari za kimanzingira zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Akitoa ufafanuzi zaidi kaimu afisa afya na mazingira wilaya ya Rungwe bwana Salum Kilanga
amesema kuwa miradi inatakiwa ianzishwe katika mazingira yanayochochea afya stawivu na siyo uchafuzi wa mazingira hususani kulima kandokando ya vyanzo vya maji na kutupa taka ovyo.
Akifunga semina hiyo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Busokelo bwana Eston Ngilangwa amesema kuwa maafisa ugani wanatakiwa kuwatembelea wanufaika wa mradi ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya kuendeleza miradi yao .
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa